Kinega

Vinega ni ndege wa jenasi Riparia katika familia Hirundinidae. Wanafanana na mbayuwayu lakini wana rangi ya mchanga na nyeupe. Mwenendo wao ni sawa na ule wa mbayuwayu. Hulichimba tundu lao katika ukingo au chungu ya mchanga. Jike huyataga mayai 2-5.
Kucha (Sylviidae)
Kucha ni ndege wadogo wa familia Sylviidae. Wanafanana na shoro, kuchanyika na kuchamsitu, na zamani wote waliainishwa pamoja katika Sylviidae. Zamani kucha wa Afrika kusini kwa Sahara waliainishwa katika jenasi Parisoma lakini sasa wamewekwa katika
Mbayuwayu
Mbayuwayu au vijumbamshale ni ndege wa familia Hirundinidae. Spishi nyingine zinaitwa kinega au kizelele. Wanafanana na teleka lakini hawa wamo katika oda yao yenyewe Apodiformes. Mbayuwayu wana miguu mifupi kama teleka lakini mabawa yao ni mafupi zaidi
Ninga-bahari
Ninga-bahari ni ndege wa familia Hydrobatidae na Oceanitidae. Wana mnasaba na walinzi lakini ni wadogo kuliko hawa. Spishi za Hydrobatidae ni weusi au kijivucheusi na weupe kwa kiasi mbalimbali. Spishi za Oceanitidae ni weusi juu na weupe chini. Huruka
Nyigu mlanyuki
Nyigu walanyuki ni nyigu wa ukubwa wa kati wa jenasi Philanthus katika familia Philanthidae na familia ya juu Apoidea katika oda Hymenoptera ambao huwinda nyuki ili kutaga mayai juu yao. Wanatokea duniani kote isipokuwa Australia, Amerika ya Kusini na
Bata-shimo
Mabata-shimo ni ndege wa maji wa nusufamilia ya Tadorninae katika familia ya Anatidae. Mabata hawa ni katikati ya mabata wachovya na mabata bukini kwa ukubwa na kwa umbo. Wanaitwa mabata-shimo kwa sababu spishi nyingi hutaga mayai ndani ya shimo la mti au
Fuluwili
Fuluwili ni ndege wa jenasi Canirallus na Sarothrura, jenasi pekee za familia Sarothruridae. Ndege hawa wanafanana na viluwiri lakini wana rangi kali zaidi. Wanafanana nao kwa mwenendo pia
Kereng'ende (ndege)
Kereng'ende ni ndege wa jenasi Pternistis katika familia Phasianidae. Huitwa kwale pia pamoja na spishi nyingine za nusufamilia Perdicinae. Kwa sababu jenasi hiyo inatambuliwa kuwa na nasaba mbali kidogo na jenasi zile nyingine, sasa jina kereng'ende
Jurawa
Jurawa ni spishi mbalimbali za ndege wadogo za jenasi Passer katika familia Passeridae ambao wanafanana na shomoro wenye kichwa kijivu. Ndege hawa wana domo fupi na nene lifaalo kula mbegu, lakini hula wadudu wadogo pia hasa wanapokuwa makinda. Spishi
Kukuziwa
Kukuziwa ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia Rallidae. Wana mnasaba na viluwiri lakini ni ndege wa maji wa kweli. Wanaachana na viluwiri kwa kuwa na kigao kidogo juu ya domo. Rangi yao ni nyeusi au kijivu nzitu na mabawa ya spishi nyingi yana
Tunguhina
Tunguhina ni ndege wadogo wa jenasi Uraeginthus katika familia ya Estrildidae ambao wana rangi kahawianyekundu na viraka buluu au zambarau. Kuna spishi tatu zingine kwa jenasi hii ambazo zinaitwa vitenduli na zina rangi buluu. Wataalamu wengine wanaweka